MKUU wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsele ameagiza watu wanaoishi bila kufunga ndoa kupelekwa mahabusu kwa kuwa watu wamekuwa wakiishi kwa muda mfupi na kupata watoto na kuachana huku wakisababisha watoto wa mitaani.
Akiwa katika Kongamano la Wanaume lenye lengo la Kupinga Mila potofu amesema watu wasiofunga ndoa wanaongeza watoto wa mtaani kwani wanakaa, wanazaa na mwisho wa siku wanaachana na kuacha Watoto wa mtaani.
Amesema; “Hizi ‘Lock Up’ zimetengenezwa kwa ajili ya nini? Wahalifu kama hao. Huyo ni Mualifu. Na kwenda ‘lock Up’ ni kawaida tu kwani lile ni jengo na ni la Serikali limejengwa litumike, likilala bila mtu ni hasara. Matumizi mabaya ya pesa ya Umma.”
Aidha, amebainisha; “Ukishakuwa na ndoa na iheshimiwe, kuwa kwenye ndoa maana yake wote ni sawa. Kuwa kichwa cha nyumba haimaanishi hauwajibiki kuleta chakula, kwenda shamba, kutunza watoto na mke au kuleta nguo za mama na watoto nyumbani.”
Amesisitiza, “Kuwa kichwa maana yake Watoto wapate chakula, waende shule na uwalipie wapate chakula shuleni. Pia ununue sare za Watoto za shule.”
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments