Familia Yakaa Chini ya ARDHI Miaka 9 ikisubiri Mwisho wa Dunia | ZamotoHabari.



Leo October 17, 2019 Polisi nchini Uholanzi imegundua chumba cha siri cha chini ya ardhi kilichokuwa kikitumika na familia moja kwa zaidi ya miaka tisa.

Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa chumba hicho kimegunduliwa Jumanne October 15 na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu.

Familia hiyo ilikuwa ikiishi chini ya ardhi kwa muda wa miaka tisa kwa kile walichodai kuwa ilikuwa ikisubiri siku ya mwisho wa dunia.



Shirika la Utangazaji la BBC, liliandika kuwa mwanaume wa miaka 58 na watoto wake sita walio na umri kati ya miaka 16 hadi 25 walikuwa wakiishi katika chumba hicho kilichopo katika shamba lao katika lililopo katika Mkoa wa Kaskazini wa Drenthe.

“Walipatikana baada ya kijana wake mkubwa kuenda kununua pombe katika baa moja karibu na kijiji cha Ruinerwold na kumfahamisha mhudumu wa kwamba anataka usaidizi,” kituo cha Televisheni cha RTV kiliripoti.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini