FBI Yamtambua Mhalifu Hatari Zaidi Marekani | ZamotoHabari.


FBI imetoa michoro ya Samuel Little ili kusaidia utambuzi wa waathiriwa
Shirika la upelelezi la Marekani FBI limethibitisha kuwa mfungwa muuaji amekiri kuwaua watu 93 miongo minne iliopita ni mhalifu hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Polisi imemhusisha Samuel Little na mauaji ya watu 79 katika visa 50 vya uhalifu wa aina hiyo kutoka mwaka 1970 hadi 2005 kufikia sasa.

Amekua akihudumia kifungo cha maisha gerezani tangu mwaka 2012 baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya wanawake watatu.


Little aliwalenga hususan wanawake weusi ambao baadhi yao walikua makahaba na watumiaji wa dawa za kulevya, maafisa wanasema.

Bondia huyo wa zamani alikuwa akiwapiga ngumi waathiriwa wake kabla ya kuwanyonga - kumaanisha mara nyingi hakuna ushahidi wa "kudhibitisha" kuwa mtu aliuawa kikatili.

Baadhi ya vifo hivyo havikuchunguzwa na FBI na vingine vilidhaniwa kutokana na ajali au sababu zingine. Miili mingine haikuwahi ikipatikana, shirika hilo linasema.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumatatu, FBI ilisema wachunguzi wake wanaamini ushahidi wake "wote ni wa kweli".

"Kwa miaka mingi, Samuel Little aliamini hatawahi kujulikana kwa sababu hakuna mtu aliwatafuta waathiriwa,"mchambuzi wa masuala ya uhalifu wa FBI, Christie Palazzolo alisema katika taarifa hiyo.

"Japo tayari ni mfungwa, FBI inaamini ni muhimu kuwatafutia haki waathiriwa - wa karibu kila kesi."

Maafisa wa usalama bado wanachunguza visa 43 vya mauaji aliyokiri kutekeleza
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini