Kocha Simba SC Aisifu Beki Yake | ZamotoHabari.


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amekoshwa juu ya maendeleo ya pacha ya mabeki wake Muivory Coast, Pascal Wawa na Mbrazili Tairone Santos kwa kucheza mechi tatu sawa na dakika 270 za karibuni bila ya kuruhusu timu yao kufungwa bao lolote.



Pacha hiyo ya mabeki hao ilicheza kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambayo Simba walishinda mabao 3-0 kisha dhidi ya Biashara United mabao 2-0 na wakacheza kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Bandari ambayo walishinda kwa bao 1-0.



Aussems ameliambia Championi Jumatano, kuwa mabeki wake hao wamekuwa wakifanya vizuri na wanaelewana kwa sasa tofauti na zamani ndiyo maana wameweza kucheza kwa muda huo bila ya kuruhusu bao lolote wao kufungwa.



“Huwezi kusema wanafanya makosa kwa sababu hadi sasa hatujafungwa bao kwenye mechi ambazo Wawa amecheza na Tairone. Kitu kizuri ni kuwa wanaendelea kucheza kwa kuelewana kwa kadiri siku zinavyokwenda. “Lakini siwezi kusema kwamba wao ndiyo wataendelea kucheza kila mara kwa sababu hapa kuna wachezaji sita ambao wana uwezo wa kucheza nafasi hiyo.



Muda mwingine ninaweza kuwapanga Kennedy Juma na Mlipili (Yusuph) na wengine na bado wakacheza na tukapata matokeo mazuri lakini hawa wananifurahisha,” alisema Aussems.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini