Kwa Maneno ya KUCHOMA Moyo...Majizzo Afunguka Kuhusu Maulid Kitenge Kuhamia Wasafi FM | ZamotoHabari.

"Umekuwa wakati mzuri sana kwenye tasnia ya habari na burudani haswa kwa Familia ya EFM Radio na TVE kuwa na Mtangazaji na Kiongozi wa namna yako. “CHUMVI” @kitengemaulid .

Kwa dhati kabisa tunashukuru kwa mchango wako na matumizi mazuri ya taaluma yako katika kuupasha habari Uma wa Watanzania. Miaka mitano kwa Efm naamini ni muda mzuri uliotosha kukujenga, kuwapa hamasa vijana wengine, kujifunza vitu vipya na kuwa miongoni mwa Timu kubwa iliyofanya Taasisi ya EFM na TVE kufika hapa tulipo. .

Uongozi wa Efm unakutakia kila lenye kheri katika mapambano na majukumu yako mapya. Tunaamini hautatuangusha katika utendaji wako kama ilivyo desturi yetu “HATUPOI, HATUBOI” cc @efmtanzania @tvetanzania" Ameandika DJ Majizzo
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini