Mama Diamond Afunguka Kwa MARA ya Kwanza Kuhusu Mtoto wa Tanasha Kuwa Mwarabu | ZamotoHabari.



Mama Dangote aamua kufunguka baada ya maneno kuibuka mitandaoni kuwa mtoto wa Tanasha Baba ake sio Diamond wakidai hawafanani mtoto nywele zake yupo kama Mwarabu.

Habari kutoka kwa chanzo cha gazeti la Amani, kilicho ndani ya familia ya Mondi zinadai kuwa, kutokana na madai hayo, wapo baadhi ya ndugu nao wanashinikiza kifanyike kipimo cha DNA ili kumaliza utata huo.

“Ni kweli hiyo ishu imeleta sintofahamu baada ya mama Diamond kutupia vipande vya picha za mtoto huyo zinazoonesha sehemu ya kichwani. Wapo wanaodai yule mtoto ana nywele za Kiarabu na wengine wanadai ni Singasinga hivyo kitakachong’amua kitendawili hicho ni vipimo vya DNA tu,” kilidai chanzo hicho

Amani lilipozungumza na Mama Dangote kumuuliza kuhusu madai hayo na kama ni kweli familia inashinikiza kupima DNA? ambapo Mama Dangote alijibu kwa kifupi kwa kusema

"Na sisi tunaona tu kama ninyi mnavyoona mitandaoni, Kwa hiyo subirini mtaona.”

Amani: Tusubiri tutaona akibadilika na kufanana na Diamond au?

Mama Dangote: Mimi ninachowaambia subirini mtaona.

Hata hivyo, madai hayo yameibuka mitandaoni huku ikijulikana wazi kuwa Tanasha ni mchanganyiko wa wazazi wenye asili ya Afrika na bara Asia.

Ikumbukwe pia kwa Princess Tiffah madai kama haya yaliwahi kuibuka kuwa sio mtoto wa Diamond Platinumz

Nini maoni yako
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini