Wanariadha kutoka Tanzania Faraja Damas na Joseph Panga wamefuzu kuingia fainali ya Mita 5000 katika mashindano ya majeshi ya dunia yanayoendelea nchini China huku akiwapita wanariadha wengine 47.
Faraja alishika nafasi ya kwanza baada ya kukimbia kwa dakika 14:39.24 huku akiwaacha nyuma wakimbiaji wengine katika kundi la pili la wakimbiaji waliokuwa wakisaka nafasi ya kuingia fainali.
Hata hivyo siku ilikuwa Njema kwa mwanaridha Joseph Panga baada ya kufuzu katika hatua ya Fainali baada ya kukimbia nafasi ya sita kwa dakika 14:10.47 ambazo zilizidi mshindi wa kundi la kwanza na kupata nafasi kuingia fainali.
Katika kundi la kwanza Mkenya Peter Ndegwa aliongoza baada ya kukimbia kwa dakika 14:04.67 na kufanikiwa kutinga fainali huku akiwa na kibarua cha kukabiliana na wanaridha wengine 14 waliofuzu mbio za Mita 5000 kOktoba 26 ili kumpata mshindi wa kwanza wa pili na watatu .
Wakati huo Mwanariadha Private Magdalena Shauri aliyeshinda mashindano ya afrika mashariki ya majeshi ameshindwa katika fainali za mbio za Mita 5000.
Sasa huku wanariadha wa Marathoni wakiongozwa na Private Felix Simbu wakitarajiwa kukimbia tarehe 27. Wakati huo huo bondia selemani kidunda ametolewa katika hatua ya robo fainali baada mpambano mkali ambapo kidunda alipambana muda wote na kumrushia mpinzani wake makonde mazito. Hata hivyo mpaka mwisho wa Mpambano Kidunda alipata pointi 26 huku mpinzani wake Ghousoon Ahmad wa syria akipata pointi 30 na kutangazwa mshindi baada ya maamuzi ya majaji wote watano.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments