Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akimkabidhi mashuka kwa Muuguzi wa Zahanati ya Kata ya Shelui, Cecilia Emmanuel alipokuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Diwani wa kata hiyo Kinota Khamis (JB)
Mhe.Aysharose Mattembe akisaini katika kitabu cha wageni katika Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata ya Shelui Kinota Khamis akitoa taarifa fupi kuhusu zahanati hiyo. Kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu wa kata hiyo, Jenipher Miano.
Muuguzi wa zahanati hiyo, Cecilia Emmanuel akisoma taarifa fupi ya zahanati hiyo mbele ya Mbunge Mhe. Aysharose Mattembe.
Mhe.Mattembe akizungumza na wagonjwa waliokuwepo kwenye zahanati hiyo kupata matibabu.
Mhe Mattembe akigawa sabuni kwa wagonjwa.
Mhe.Mattembe akimpatia sabuni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Alex Paulinus (wa pili kulia) kwa niaba ya watumishi wenzake.
Hapa Mhe. Mattembe akikagua chumba cha maabara.
Diwani wa Kata hiyo, JB akizungumza na wanawake waliowapeleka watoto wao kliniki katika zahanati hiyo.
Mhe. Mattembe akizungumza na wanawake waliowapeleka watoto wao kliniki katika zahanati hiyo.
Mhe.Mattenbe akiwakabidhi mashuka wanawake hao kwa ajili ya zahanati hiyo.
Mhe.Mattenbe akiwakabidhi mashuka wanawake hao kwa ajili ya zahanati hiyo.
Majengo ya zahati mpya iliyoanza kujengwa kwa msaada wa Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ambao ujenzi wake umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANANCHI wa Kata ya Shelui Wilayani Iramba mkoani Singida wameiomba Serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kata hiyo ili waondokane na adha wanayoipata ya kupata huduma za matibabu
Wananchi hao walitoa ombi hilo kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata hiyo mwishoni mwa wiki.
Akizungumza mbele ya mbunge huyo mkazi wa Kijiji cha Kibigiri Mussa Kizugulu alisema wanachangamoto kubwa ya kutokuwa na zahanati kwani iliyopo ni ndogo na inaelemewa na wingi wa watu wanaokwenda kupata huduma.
Alisema zahanati hiyo inatoa huduma kwa wananchi kutoka Kijiji cha Kisonso ambacho kipo kilomita 10, Masagi kilometa nane, wembere kilometa tisa na Tintigulu kilometa nane ambao hulazimika kutembea umbali huo hadi kufika katika zahanati hiyo kupata matibabu.
Mwadawa Salum kutoka Kijiji cha Nselembwe alisema changamoto nyingine waliyonayo ni pale inapotokea ajali katika barabara kuu ya kutoka Singida kwenda Mwanza ambayo inapita jirani na zahanati hiyo kuwa watumishi huzidiwa kutoa matibabu na kulazimika kuwapeleka majeruhi Igunga na Tabora kwa matibabu.
Mkazi wa Kijiji cha Kyala Mwajuma Permena alisema zahanati hiyo kwa sasa imezidiwa hivyo kuwa changamoto kwa wajawazito wanaokwenda kujifungua kutokana na chumba cha wazazi kuwa kidogo.
Diwani wa kata hiyo Kinota Khamis (JB) alisema jengo la zahanati hiyo ni chakavu kwani lilijengwa toka enzi ya ukoloni mwaka 1937 lakini mwaka 2010 Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alianza kuwajengea zahanati nyingine ambayo ujenzi wake bado haujakamilika ambapo anaiomba serikali iwasaidie kukamilisha ujenzi huo na kuifanya zahanati hiyo kuwa kituo cha afya ili kuwapunguzia adha wananchi.
Mbunge Aysharose Mattembe baada ya kuambiwa changamoto hiyo aliahidi kuifanyia kazi kwa kuwapelekea wahusika ambapo pia alitoa mashuka kwa ajili ya zahanati na sabuni ambazo alizigawa kwa wagonjwa na watumishi wa zahanati hiyo.
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments