Meya Aburuzwa NYUMA ya Gari Kwa Kutotimiza Ahadi za Uchaguzi | ZamotoHabari.


Mexico: Watu 11 wamekamatwa kwa kosa la kumkamata Meya wa Las Margaritas katika Jimbo la Chiapas, Jorge Luis Escandón Hernández kisha kumfunga katika gari na kumburuza katika mitaa mbalimbali

Polisi walifanikiwa kumuokoa Meya huyo ambaye alipata majeraha. Hili ni shambulio la pili kutoka kwa Wananchi ambao wanadai Meya Hernández hajatimiza ahadi alizotoa, ikiwemo ujenzi wa barabara

Meya pamoja na viongozi wa chini wa Serikali mara nyingi hushambuliwa nchini Mexico na makundi ya kihalifu wasipofanya matakwa wanayoyataka, lakini kupigwa kutokana na ahadi za uchaguzi ni jambo geni

Video zilizochukuliwa na wapita njia nje ya ofisi ya Meya huyo na kusambaa mtandaoni zimeonesha kundi la Wanaume wakimvuta nje ya jengo na kumfunga nyuma ya gari na kumburuza katika mitaa ya Santa Rita

Huku Meya Hernández akisema atafungua kesi ya kutekwa na kutaka kuuwawa kutokana na tukio hilo, itakumbukwa kuwa miezi kadhaa iliyopita watu wasiojulikana walivamia na kuharibu ofisi yake, lakini yeye hakuwepo
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini