Mkurugenzi wa zamani Mipango Takukuru, aomba aomba msamaha yuko tayari kulipa | ZamotoHabari.

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MKURUGENZI wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Mansoor, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, ameandika barua kwa DPP kwa ajili ya kukiri kosa katika kesi uhujumu uchumi inayomkabili.

Akiwasilisha taarifa hiyo, mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina, wakili wa mshtakiwa huyo, Eliya Mwingira amedai, mteja wake ameishaandika barua kwa DPP hivyo ni vema wakapata majibu kwa wakati ili mshtakiwa aweze kupata haki yake ukizingatia kuwa ameishakaa gerezani kwa muda mrefu, tunaomba japo tarehe ijayo tuwe tumepata majibu.

Mapema, wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai kuwa, kesi hiyo leo Oktoba Mosi, 2019 ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi  bado haujakamilika.

Amedai watafuatilia taarifa hiyo kwa DPP na watakuja na majibu mapema.

Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 16, mwaka huu 4, mwaka huu

 Katika kesi hiyo, mshtakiwa Kuluthumu   anakabiliwa na mashitaka manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshtakiwa alighushi barua ya ofa ya  Agosti  13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya  ya Bagamoyo huku akijua kuwa sio kweli.

Katika shtaka la pili, inadaiwa  kati ya Januari 2012 na Mei 2017  huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja  kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Mansoor alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.


Mshtakiwa huyo pia  alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika shtaka la tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh milioni saba kutoka jwa Ekwabi Majungu  ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Pia anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika shtaka la utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa  alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa  fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini