Mwanajeshi mmoja wa Urusi amewapiga risasi wanajeshi wenzake wanane na kuwajeruhi vibaya wengine wawili katika kambi ya kijeshi iliopo mashariki, kulingana na maafisa.
Ramil Shamsutdinov ambaye amekamatwa huenda alikuwa akiugua tatizo la kiakili , wanasema.
Tukio hilo lilifanyika katika kitengo cha kijeshi nambari 54160 katika kijiji cha Gorny , sio mbali na mji wa Chita, siku ya Ijumaa jioni.
Wizara ya ulinzi mapema ilisema kwamba risasi zilifyatuliwa wakati wa kubadilishana zamu katika eneo la Transbaikal.
Bwana Shamsutdinov , kurutu, aliwaua maafisa wawili na wanajeshi wenzake sita.
Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kwamba mshukiwa huyo aliwalenga waathiriwa katika vichwa.
Tume maalum inayoongozwa na naibu waziri wa ulinzi Andrey Kartapolov inaelekea katika eneo hilo ili kuchunguza mauaji hayo.
Kitengo hicho cha jeshi nambari 54160 kinahifadhi makombora.
Kina makombora ya Iskander ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya kinyuklia.
Huduma za jeshi ni lazima nchini Urusi kwa wanaume wote walio kati ya umri wa miaka 18-27.
Wao uhudumu kwa miezi 12 , na baadaye wanaweza kusaini kandarasi za kitaalam ili kuendelea kuhudumu katika jeshi.
Katika miaka ya 2000, makundi ya haki za kibinadamu yaliripoti ghasia na unyanyasaji kwa jina ''dedovshchina'' dhidi ya makurutu wapya katika jeshi la Urusi.
Lakini katika miaka ya hivi karibuni, Urusi inajivunia kuliimarisha jeshi lake na kuondoa unyanyasaji.
Facebook
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments