Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema hana wasiwasi endapo atafukuzwa kazi kunako klabu hiyo.
Taarifa imesema Zahera ambaye ni raia wa Congo ameeleza hana wasiwasi sababu ana ofa nyingi mezani ambazo anaweza akazitumia.
Ameeleza kuwa kufukuzwa ni sehemu ya kazi kwani makocha wengi huajiriwa na kufukuzwa hivyo kwake si jambo geni.
Kumekuwa na tetesi za Zahera kuondoshwa Yanga kutokana na aina ya matokeo ambayo amekuwa akiyapata haswa baada ya kipigo cha juzi dhidi ya Pyramids FC ya Misri.
Tetesi zilizopo hivi sasa ni kuwa inaelezwa Yanga wanaweza kumrejesha kocha wao wa zamani Hans van der Pluijm ama Kim Poulsen.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments