Ndugu Waanza Kutambua Maiti ya Ajali ya Gari iliyoanguka Katika Daraja Handeni | ZamotoHabari.


Miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali iliyotokea katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga  imeanza kutambuliwa na ndugu zao.

Gari waliyokuwa wanasafiria lilianguka katika daraja  lililokatika kutokana na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha mkoani humo.

Jitihada mbalimbali zinaendelea ili kuhakikisha barabara ya Kilindi Handeni inafunguka na kikosi jeshi cha 121 kutoka Ngerengere kimeanza kuleta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa madaraja yaliyokatika.

Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe amesema kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo imeongezeka na kufikia watu 12 baada ya kupatikana kwa miili miwili.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini