RC SINGIDA AKUTANA NA MAMA MASHUJAA WA CHAKULA WA OXFAM KATIKA MAONESHO YA CHAKULA | ZamotoHabari.

 Mama Shujaa wa chakula kutoka Shirika la Oxfam, Stella Masulya akimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi namna ya anavyohofadhi samaki wake kwa kutumia moshi na anavyoandaa dagaa kwa njia ya asili katika maonesho ya kuadhimisha siku ya chakula duniani yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Singida.
 Dkt.Nchimbi akisaini katika kitabu cha wageni katika banda la Oxfam kwenye maonesho hayo.
 Mama Shujaa wa chakula kutoka Arusha, Elinuru Moses akimuelezea Dkt. Nchimbi umuhimu wa kutumia vyakula asilia na namna ya kuvihifadhi.
 Wakina mama Shujaa wa chakula kutoka mikoa mbalimbali walioshiriki maadhimisho ya siku ya chakula duniani wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
 Dkt.Nchimbi akipokea zawadi ya viazi lishe vinavyozalishwa na wakulima wadogo wadogo kutoka Mbongwe.
 Mama Shujaa wa chakula kutoka mkoani Mtwara akimuuzia vikapu Dkt. Nchimbi alivyotengeneza kama mjasiriamali mdogo ili kukuza kipato cha familia yake.
Mama Shujaa wa chakula, Elinuru Moses akimuelekeza Dkt. Nchimbi umuhimu wa chakula asilia  katika kuboresha afya.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini