Serikali imesema ipo tayari kulipa Deni la shilingi Bilioni 13 kwa wakulima wa korosho Wilayani Tandahimba.
Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo wakati akijibu maswali na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu
"Msema kweli mpenzi wa Mungu,tulishindwa kuendelea kuwalipa kwakuwa fedha ilituishia,lakini Sasa tumeshapata fedha baada ya kuuza korosho zetu zote tan220,000 kwaiyo fedha tunayo tunauhakika wa kuwalipa wakulima,"alisema Mgumbo
Alisema serikali inatarajia kulipa madeni kwa wakulima na vibarua Tanzania nzima shilingi Bilioni 89 ambazo zipo.
"Utaratibu utafanyika katika malipo hayo lakini fedha kwa Sasa ipo,sababu tulikuwa tunalipwa kwa malipwani yaani mzigo upakiwe kwenye meli ndipo malipo yafuaate kwaiyo tumemaliza zoezi hilo ," alisema Mgumbo
Aidha alisema maghala yapo wazi tayari kwa kupokea mzigo mpya hivyo muda wowote wataanza kupokea korosho kutoka kwa wakulima
Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo na Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akipata maelezo kutoka kwa mkulima Ahmad UlenjeNaibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo akifafanua jambo wakati akijibu maswali na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu
,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba .
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments