Operesheni za kutafuta miili ya Mama na Mwanaye waliozama siku ya Septemba 29, 2019 katika feri ya Likoni Nchini Kenya, zinaendelea kwa vikosi vya Serikali, Sekta binafsi na vikosi kutoka Afrika Kusini vikishirikiana
Uwepo wa Vikosi vya wazamiaji wa Afrika Kusini umeongeza nguvu lakini kina cha bahari, vifaa visivyo na ubora pamoja na uonaji usio mzuri ni changamoto kubwa katika uokoaji huo
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Huduma katika Feri hiyo amesema, timu ya wazamiaji kwa sasa itategemea zaidi teknolojia kusaidia kutambua vitu chini ya bahari na kupata mwili wa Mariam Kighenda (35) na mwanaye (4)
Mariam na mwanaye wamefariki baada gari lao kuteleza kutoka kwenye kivuko na kuzama baharini wakati wakivuka bahari kwa kutumia kivuko cha MV Harambee kilipokuwa kinakaribia kuweka nanga kisiwani
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments