UBALOZI WA CHINA NCHINI WASHEHEREKEA MIAKA MITANO YA MASHAURIANO YA KISHERIA YA NCHI ZA AALCO | ZamotoHabari.

UBALOZI wa china nchini umeadhimisha miaka mitano ya ushirikiano wa masuala ya sheria kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) jijini Dar es Salaam jana usiku.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka mitano ya mashashauriano ya kisheria kati ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) jijini Dar Es Salaam jana usiku, Waziri wa Katiba na sheria, Agustine Mahiga  alisema kuwa mashirikiano hayo yameongeza ushirikiano wa nchi ya za AALCO.

Alisema  kuwa nchi ya china pia imesaidia Tanzania katika kusomesha Viongozi, wataalamu mbalimbali pamoja na wanafunzi kwenye masuala ya kisheria.

"Wengi huwa wanajiuliza uhusiano huu ulianzaje anzaje nimeeleza kwa kufupi Mwaka 1963 kulikuwa na maasi ya Jeshi Miaka Miwili tuu baada ya uhuru lile jeshi letu lilikuwa dogo lakini lililuwa la kikoloni na maafisa wake walikuwa wa kikoloni walipigana vizuri huko Bama na katika Ushindi na walipo rudi makao ya jeshi hapa Kawe yakapewa jina la Kolito Balax kwa sababu ushindi walioupata huko Visinia kwa sababu ushindi walioupata huko ulikuwa katika uwanja wa vita uliokuwa ukiitwa Kolito lakini pale Kolito balax leo panaitwa Lugalo pameitwa jina la ushindi la wa wahehe dhidi ya Wajerumani. Alisema Mahiga.

Hata hivyo Mahiga alielezea kuwa walipoleta maasi mwaka 1963 hayakufanikiwa lakini Hayati Mwalimu Julius Nyerere akaamuru kuundwa jeshi jipya ambapo akaomba wachina kusaidia kujenga jeshi jipya ndio maana leo tunajeshi la Wananchi (JWTZ).

"Hilo ndio likawa chimbuko la Urafiki wa Tanzania na China lakini kwa hilo na sisi tukaona hawa wametuitikiwa wakati wa shida lakini na wao walikuwa na shida kubwa kwani walikuwa wametengwa kimataifa, walikuwa hawapo kwenye umoja wa mataifa". Alisema Mahiga. 

Mahiga Alielezea kuwa Mwalimu Nyerere alisema kuwa kama tunataka kujenga mfumo wa usawa mbele ya umoja wa mataifa atakwenda kuwaambia kwasababu walitusaidi sisi na sisi tuisaidie china  ichukue kiti chao katika umoja wa mataifa.

Alisema kuwa Tanzania ilisaidia nchi ya China kupata kiti chao cha kudumu katika barazabaraza la usalama.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Balozi Agustine Mahiga akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka mitano ya mashauriano ya kisheria wa nchi za Asia na Afrika (AALCO) jijini Dar es Salaam jana usiku.
Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke akizungumza wakati wa kusheherekea miaka mitano ya mashauriano ya kisheria kati ya nchi za Asia na Afrika ambayo imefanyika jijini Dar es Salaam jana usiku.
Katibu Mkuu wa Shirika la Mashauriano ya kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO), Kennedy Gastorn akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka mitano ya mashauriano ya kisheria kati ya nchi za Asia pamoja na nchi za Afrika jijini Dar es Salaam jana usiku.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Balozi Agustine Mahiga na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke wakizungumza mara baada ya kugonganisha glasi wakati wa sherehe za kusheherekea miaka mitano ya mashauriano ya kisheria kati ya Nchi za Asia na nchi za Afrika.
Picha ya pamoja.


Baadhi ya wageni waalikwa.


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini