Yanga Kutua Mwanza Leo Waandaliwa Mapokezi Babu kubwa | ZamotoHabari.


YANGA inatua hapa Mwanza kesho Ijumaa na uongozi wa matawi yao jijini hapa umewaandalia mapokezi ya maana.



Katibu mkuu wa matawi hayo, Mhando Madega amesema; “Tulikuwa na kikao na viongozi wa matawi ya Yanga jijini Mwanza kwa pamoja tumeazimia kuipokea timu yetu kwa mapokezi makubwa ikiwa ni ishara ya kufanya vyema katika michezo yetu miwili dhidi ya Mbao na Pyramids.”



“Licha ya kuandaa mapokezi makubwa lakini sisi hatulali tunapambana ili Yanga yetu iweze kupata matokeo ya hii michezo miwili kwani endapo tutafanya vizuri katika michezo yetu yote tutajenga imani kubwa kwa viongozi wetu wa juu waendelee kutuamini ili hata michezo mingine waweze kuileta katika jiji la Mwanza ambako tunapata matokeo,”alisema
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini