Daktari Bingwa wa Kina Mama Awatoa Wanawake Vizazi Bila Ridhaa Yao | ZamotoHabari.

Daktari mmoja anatuhumiwa kwa kufanya upasuaji kwa wanawake na kutoa viungo bila ridhaa zao, mmoja wa wagonjwa wake amemtuhumu na kumfikisha mahakamani.

Amefikishwa katika mahakama huko Virginia nchini Marekani.

Dr Javaid Perwaiz dakatari bingwa wa kina mama, amewadanganya wanawake kuhusu afya zao na kuwasababishia majeraha makubwa, kwa mjibu wa shirika la upepelezi la marekani FBI.

Tangu kukamatwa kwake tarehe 8 novemba , zaidi ya wanawake 126 wameripoti na kulalamika kuhusu tabia zake.

Siku ya alhamisi , jaji wa mahakama alitoa amri ya kukamatwa kwa Dr Perwaiz wakati akisibiri hukumu yake.

Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa ya FBI Dr.Perwaiz anatuhumiwa kutoa majibu ya uongo ya kiafya na kufanya upasuaji usio wa lazima kwa wagonjwa wake na bila ridhaa zao.

Unaweza pia kusoma

Vitu gani hutufanya kuwa na uraibu?
'Nilikabiliwa na uraibu wa ngono kwa miaka sita'
'Sikutosheka kushiriki ngono mara 5 kwa siku'
Amefanya upasuaji wa kutoa sehemu za uzazi za wanawake bila ridhaa zao pamoja na kufunga uzazi. Daktari huyo ana ofisi mbili eneo la Chesapeake, jimbo la Virginia nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa mahakamani, katika kipindi cha mwaka 2014-18 Dr Perwaiz amefanya upasuaji kwa asilimia 40 ya wanawake wanaopokea matibabu wakiwa na kipato cha chini.

Katika kundi la wagonjwa wanawake 510,asilimia 42 walifanyiwa angalau upasuaji wa aina mbili.

Shirika la upepelezi la FBI lilipewa taarifa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na muuguzi ambae alisikia kutoka kwa mgonjwa mmoja.

''Wagonjwa wanasema kuwa walikua wakisikia Dr Perwaiz akitaja sana kuhusu saratani na kuwatisha waweze kufanyiwa upasuaji'' anasema Afisa wa FBI Desiree Maxwell.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Daktari huyu amekua akiwafunga vizazi wanawake bila ridhaa zao.
Wakili wa Dr Perwaiz hakujibu baada ya kutafutwa na BBC siku ya Alhamisi.

Dr Perwaiz amesoma masomo yake ya utabibu huko Pakistani na alipata leseni ya kufanya kazi Virginia Marekani mwaka 1980.

Mwaka 1982 alipoteza sifa zake za kufanya kazi katika hospitali huko Maryland kutokana na maamuzi mabaya ya kitabibu.

Kwa mujibu wa FBI alifanyiwa uchunguzi mara ya kwanza na bodi ya madaktari wa Virginia kwa kufanya upasuaji bila kuwa na maamuzi yasiyo na weledi wa kitaaluma.

Baada ya kukubali hatia ya kukwepa kodi 1996, alinyang'anywa leseni kwa miaka miwili.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini