Msanii wa muziki nchini, Gigy Money, amesema hakumbuki mara yake ya mwisho kutumia kinga, wakati wa kufanya mapenzi.
Gigy Money amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya ku post picha katika mtandao wa Instagram, ambayo inasema watu wengi wanapofanya mapenzi huwa hawatumii kinga
"Sikumbuki mara ya mwisho kutumia kinga ila nakumbuka mara ya mwisho kupima na nilipima mwezi ulioisha tu hapo, majibu yalikuwa vizuri tu ila nilishawahi kutumia kinga tena ikiwa sikuamini, kama hatujawahi kupima pamoja, hatujajuana au nikiangalia hulka yako huwa nakuacha tu maana sipendagi kuchoshana" ameeleza Gigy Money.
Aidha Gigy Money amesema, hawezi kumtaja mtu ambaye aliwahi kutumia naye kinga kwa sababu si mtu maarufu na hakuna mtu anayemjua na hata akimtaja haisaidii kitu.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments