Dar es Salaam. Verdiana Mjwahuzi (80), mama mzazi wa mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera, amefariki dunia leo Jumanne Desemba 31, 2019 familia imethibitisha.
Taarifa kutoka kwa wanafamilia imesema marehemu Verdiana amefariki akiwa anapata matibabu katika Hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Erick ambaye kwa sasa yuko rumande katika gereza la Segerea, Dar es Salaam, alikamatwa Julai 2019 kwa makosa ya utakatishaji fedha, kukwepa kodi na kushiriki katika genge la uhalifu. Alipokamatwa alikuwa akiishi na mama yake.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments