VITUO 145 KUTUMIKA KUANDIKISHA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA NAMTUMBO. | ZamotoHabari.

NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO.

Jumla ya vituo 145 vinatarajiwa kuanza kutumika katika wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma katika zoezi la kuandikisha vitambulisho vya kupigia kura linalotarajiwa kuanza Kesho tarehe 30 mwezi desemba mwaka huu.

Akiongea kwenye mafunzo na waandishi wasaidizi pamoja na waendesha mashine ya kutolea vitambulisho katika ukumbi wa shule ya sekondari Nasuli Ofisa uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Ebehard Haule alisema kuwa kazi ya uandikishaji inahitaji umakini mkubwa ili kazi iweze kufanyika kwa ufanisi.

Bwana Haule aliwataka watumiaji wa mashine na wasimamizi kushiriki mafunzo hayo kwa makini na kwenda kufanyakazi kwa weledi wa hali ya juu na kuleta ufanisi wa kiwango cha juu katika vituo vyote vya uandikishaji.

Hata hivyo bwana Haule aliwatahadharisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa ,kutouliza maswali kwa wataalamu wanaotoa mafunzo katika maeneo ambayo yatawapa shida katika kuendesha mashine za kutoa vitambulisho itasababisha kuleta usumbufu wakati wa uandikishaji ni heri ukauliza na kujiridhisha maeneo yote yanayowatia mashaka katika uendeshaji mashine hizo kabla ya kukabidhiwa mashine na kufika kituo cha kazi.

Afisa Tehama wa wilaya ya Namtumbo bwana Edwin Swai aliendesha mafunzo ya siku mbili kwa watumiaji wa mashine ya kutolea vitambulisho vya kupigia kura huku akiwataka kwenda kufanya kazi kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa katika mafunzo hayo ili kuleta ufanisi katika kazi.

Pamoja na hayo,Swai aliwataka watumiaji wa mashine hizo kutoingiza password za kwao kwa madai kuwa wapo baadhi ya watumiaji wa mashine hizo katika Halmashauri hiyo hufanya majaribio ya kuingiza password za kwao alisema swai.

Wataalamu 6 wa mifumo kutoka ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi walihusika katika kuhakikisha mafunzo hayo wanatolewa na kufuatilia kwa washiriki kuona changamoto na kuzitatua kwa vitendo katika ukumbi huo wa Nasuli.

Wataalamu kutoka tume alikuwa Mwitalu Keboya,Bertha Blandes,Edward Kombe,Mwamkai Nombo ,Eloi Laban na Abdulaziz Kingolile ambao kwa pamoja walisaidia kutoa mafunzo kwa vitendo kwa watumiaji wa mashine za kutolea vitambulisho vya kupigia kura .

Joseph Watua ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo alisema amefarijika sana kwani anaamini anaenda kufanya kazi kwa uhakika kutokana na namna alivyoelewa kwa vitendo namna ya kutumia mashine hizo kutokana na mafunzo hayo.

Wilaya ya Namtumbo inajumla ya vituo vya uandikishaji wapiga kura 145 ambapo watumiaji wa mashine za kutolea vitambulisho watakuwa 145 huku waandishi wasaidizi watakuwa 145 na waandishi wa akiba 21 na watumiaji mashine wa akiba 21.
Watendaji wa kata wakiweka vyema maboksi yaliyo na fomu za kuandikisha wapiga kura katika kata zao
watumiaji wa mashine za kuandikisha wapiga kura


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini