Breaking NEWS: Ndege ya Ukraine yaanguka Iran | ZamotoHabari.


Ndege ya Ukraine aina ya Boeing-737 iliyokuwa na abiria 180 imeanguka Iran, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la kimataifa la ndege la Ukraine ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari katika uwanja wa ndege wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Ripoti za awali zinadai kuwa ndege hiyo ilikuwa safarini kuelekea mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Haijabainika ikiwa ajali hiyo ina uhusiano wowote na mzozo wa Iran-na Marekani.

Kikosi cha uokoaji tayari kimetumwa katika eneo la tukio karibu na uwanja wa ndege, eneo ambalo ndege lilianguka.

"Ndege imeshika moto na tumetuma kikosi huko... na tunaweza kuwaokoa baadhi ya abiria ," kiongozi wa huduma za dharura Pirhossein Koulivand,ameviambia vyombo vya habari,Reuters imeripoti.

Tutakufahamisha mengi zaidi kuhusiana na taarifa hii kadri tutakavyoipokea.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini