Huyu Ndiye Mwanafunzi Aliyepata ALAMA 7 Kwa Kupata "A" Katika Masomo Yote Tisa | ZamotoHabari.



Mwanafunzi Yohana Lameck kutoka Shule ya Kata ya Igaganulwa iliyopo mkoani Simiyu aliyewashangaza wengi kwa kupata ufaulu wa Daraja la kwanza lenye alama saba (7) huku akipata A masomo yote tisa alipotembelewa na vyombo vya habari nyumbani kwao kata ya Dutwa wilayani Bariadi.

Ufaulu wa mwanafunzi huyo uliwashangaza wengi kutokana na mwanafunzi huyo kutokea katika familia duni yenye kipato cha chini na kudaiwa wakati mwingine kutohudhuria darasani kwaajili ya kwenda kufanya vibarua ili aweze kumuhudumia mama yake Mariam Lulyalyana na bibi yake wanaomtegemea.

#HONGERA SANA
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini