Iran Yakiri Kudungua Ndege Ya Ukraine | ZamotoHabari.



JESHI  la Iran hatimaye limekiri kudungua kimakosa ndege ya abiria ya Ukraine siku ya Jumatano ya Januari 8, mwaka huu,  televisheni  ya taifa ya Iran imeripoti.

Taarifa ya jeshi la Iran  imeeleza kuwa mkasa huo umetokana na “makosa ya kibinadamu” baada ndege hiyo kupita karibu na eneo nyeti linalomilikiwa na Kikosi cha Mapinduzi (Revolutionary Guards).



Maafisa waliofanya kosa hilo wataadhibiwa, taarifa hiyo imeeleza.

Awali Iran ilikanusha vikali kuwa moja ya makombora yake yaliitungua ndege hiyo karibu na mji mkuu wa Tehran.

Watu wote 176 ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha.




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini