JE, ni Kweli ASLAY Kapotea ? Ni Kweli ASLAY Ameisha Ukali Kimziki? | ZamotoHabari.



Haya bwana Nimekaa nikaona niweke hili sawa kwa wadau.
Kwanza kabisa Aslay hakufanya kosa kutoka Yamoto band na pia kufa kwa Yamoto Band sio kosa.
Yamoto sio kundi la kwanza kufa ni kitu cha kawaida hasa pale msanii anapowaza kuwa mkubwa zaidi.

Kuvunjika kwa kundi la Yamoto kumeweza kusaidia kuona ukubwa na msanii kama solo ila pia maendeleo yake personally.

Mfano leo hii Aslay ni moja ya wasanii wenye mkwanja nzuri tu hapa bongo, vile vile mtu kama Mbosso unaweza kuona alikuwa hana gari leo anamiliki ndinga lake kali tu na mjengo mkali. Kwa namna moja au Nyingine wamepiga hatua badala ya kugawana leo wanapiga mkwanja kivyao.
Like Wise Kwa Beka na Enock maisha yanaendelea kama kawaida.
Sasa leo nafocus na Aslay. Huyu jamaaa alikuwa Yeye kabla ya Yamoto na alipiga Show kama Solo kwahiyo alikuwa mkali yeye kama yeye Kabla sema Yamoto ikampa chance ya kufanya poa zaidi. Hivyo anajua matunda ya Solo na ya Kundi

Narudia tena Aslay hakufanya kosa kosa lilikuja kwenye PROMO yake. Aslay Alipigiwa Promo kubwa kuliko ukubwa wake kitu ambacho ndio chanzo cha kumshusha. Ilifika hatua watu wanamlinganisha Aslay na watu kama Harmonize,Diamond na King Kiba hapo ndo tatizo lilikuja.
Sasa promo ikiwa kubwa kuna kuvimba bichwa na kubweteka hapo ndo tatizo linakuja. Ilifika hatua kila week Aslay alitoa ngoma baadae zikakosa mvuto ikiwa kama utoto hapo ndipo taratibu kijana akaanza kupotea kwenye mainstream na sasa yupo kawaida sana. Kitu hiki nitoe Angalizo kwa marioo_tz please musimfanyie Promo kubwa. Dogo ana uwezo wake asimame yeye kama yeye na silaha yake ya Uandishi ndio kiwe kitu UNIQUE kwake kwenye Game sio Over promotion Guys.
Aslay BADO nafasi anayo kubwa sana ambayo kwa kiasi kikubwa akitulia vizuri na akaweka mipango kazi mizuri anarudi vizuri tu.
Ingawa nina shauri Management ifanye mpango wa Aslay TOUR karibu mikoa yote akusanye Hela zake za Mwaka jana maana bado mikoani kuna Show zake nyingi zinamuhitaji.
Kwahiyo akakusanye Pesa zake then aanze kutupia mawe mengine mapya.

ASLAY NI DHAHABU INAPITA KWENYE MOTO ILI ING'AE THEN DEALS KAMA ZOTE
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini