KAILIMA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA UJENZI INAYOTEKELEZWA NA VYOMBO VILIVYOPO CHINI YA WIZARA HIYO JIJINI DODOMA | ZamotoHabari.

Mratibu na Msimamizi Mkuu wa miradi ya ujenzi ambayo inatekelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dodoma, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP Costantine Kiwone, akimweleza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima (katikati) na Maofisa wengine hatua mbalimbali za ujenzi wa nyumba za askari, Makao Makuu ya Polisi na makazi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) jijini Dodoma jana.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (katikati), akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mbaraka Semwanza (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu, Emmanuel Kayuni (wa pili kulia) baada ya kufanya ukaguzi katika ujenzi wa majengo ya jeshi hilo jijini Dodoma jana.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamhanga.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kulia), akiwa na Wakurugenzi na Maofisa wa Wizara hiyo akisisitiza jambo kwa Maofisa wa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mkoa wa Dodoma, alipofanya ziara ili kuangalia utendaji kazi na huduma zinavyotolewa kwa wananchi. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, akisalimiana na baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kabla ya kukagua ujenzi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo ambao unaendelea jijini Dodoma.

PICHA NA VERONICA MWAFISI-MOHA


Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini