Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kuanzia leo katika mikoa saba ambayo ni mikoa ya Singida, Rukwa, Mbeya, Njombe, Songwe, Dodoma na Iringa.
Taarifa ya Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuzingatia tahadhari ili kuepuka madhara mbalimbali yanayoweza kutokea.
Baadhi ya athari zinazoweza kutokea ni pamoja na makazi kuzungukwa na maji, changamoto ya usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii.
By Ally Juma.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA




0 Comments