BAADA ya kuachiwa kwa video ya wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ambao ameshirikiana na msanii bora wa kike, Faustina Charles ‘Nandy’ wenye jina la Kata, imezua utata ikionekana kutokufuata maadili hivyo kuwaweka kikaangoni wawili hao. Wimbo huo umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana kuna wadada ambao wanacheza kwenye maji wakiwa wamevalia nguo za nusu utupu. Video hiyo ilifananishwa na ile iliyowahi kumuingiza matatani msanii Snura Mushi ya Chura ambayo ilifungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).
“Hivi hawa wasanii ni akina nani hasa? Mbona kama wanadharau mamlaka zilizowekwa na Serikali? Bila shaka mamlaka husika inatakiwa kuchukua hatua hapa,” aliandika judithcharles636 kwenye Instagram juu ya video hiyo.
Baada ya kukutana na mjadala huo mitandaoni huku Dimpoz na Nandy wakiwekwa kikaangoni kwa maneno makali, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Kaimu Katibu Mtendaji wa Basata, Onesmo Kayanda ili kujua kama kuna hatua zozote zimechukuliwa dhidi ya wahusika ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Mimi siyo msemaji wa Basata, nadhani majibu kamili ya maswali hayo atakuwa nayo Katibu Mtendaji wa Basata (Godfrey Mngereza). “Nadhani tukishaiangalia ataweza kutoa majibu sahihi ya kile kinachoendelea.” Hivi karibuni, video kama hiyo ilimuingiza matata msanii Rosa Ree ambaye mwanzo alifungiwa kufanya sanaa kabla ya kuomba radhi na kufunguliwa huku akilipa faini ya shilingi milioni mbili
STORI: AMMAR MASIMBA, DAR
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments