Wengi wetu naamini tumekuwa na kajitabia kakulala na karibu na simu usiku kwenye vitanda vyetu pasipo kufahamua madhara ya kijitabia hicho.
Sasa leo ninayo mambo kadhaa yakukwambia msomaji wangu wa www.dkmandai.com kuhusu hii tabia ya kulala na simu usiku.
Zifuatazo ni faida utakazozipata endapo utaacha kulala na simu usiku kitandani kwako.
1.Utalala usinginzi mzuri na wa kutosha.
Inaaminika kuwa mtu ambaye hulala karibu na simu usiku hulala usingizi wa mang'amng'amu kwa kuwa muda mwingi huwa akihisi huenda kunasimu itaingia. Hivyo endapo kuanzia leo ukiacha kulala na simu usiku itakusaidia kulala usingizi mzuri na wa kutosha usiku.
2. Hautakuwa mtumwa wa msongo wa mawazo tena
Kwa kawaida unapolala na simu unakuwa unamawazo mengi pengine bila wewe mwenyewe kujijua huenda unawaza kwanini fulani haja kupigia usiku huo au atakupigia saa ngapi kukwambia usiku mwema hivyo unajikuta unajipatia msongo wa mawao usio na sababu na hivyo kuathiri afya yako bure. Ili kuondokana na hilo ni vyema kuweka mbali simu yako wakati wa kulala au kuweka silent kabisa.
3. Utafanya kazi / biashara zako vizuri
Kwasababu sasa unapoacha kulala na simu inamaana utapata mda mzuri na wakutosha wa kulala vizuri hivyo hata kazi zako au biashara utazifanya kwa ufanisi zaidi.
4. Utajisikia mwenye afya zaidi
Kwa sababu utakuwa unalala vya kutosha na watu wenye kulala vizuri huwa ni wenye afya.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments