Time Traveling: JE, Linaweza Kuwa Suluhisho la Kifo? | ZamotoHabari.


Mara nyingi hua nasema vitu tunavyoona ni vyakijinga havi-make sense machoni na masikioni mwetu ndio hua na maana na vimeleta mabadiriko makubwa duniani kwetu. Mfano swali la kijinga zaidi alilowahi kujiuliza mwanasayans Issac Newton leo hii limetulitea mabadiriko na maendeleo kwenye maisha , hebu fikiria kama leo hii isac newton angekuuliza kwanini apple limemuangukia kichwani halikwenda juu ungemuona vipi? Hilo swali unaloliona la kijinga limeleta maendeleo makubwa sana. Pia ndoto moja aliyoota albert Einstein waweza kuona ni ya kawaida sana au haina maana lakini ni moja kati ya ndoto iliyoleta mafanikio makubwa duniani, kupitia ndoto tu ya kawaida sana aliyoota tulipata kitu kinachoitwa Theory of Ralativity mambo ya Emc2 yote yote unaweza ona ni kitu cha kawaida ila kina impact kubwa kwenye tasnia ya sayansi

Tarehe 11/5/2019 nilibahatika kuangalia muvi hii inayoitwa Avangers: Endgame, content iliyomo kwenye muvi hii ni Time Traveling, baada ya kuangalia muvi I really admitted that Death might no longer a threat to Mankind!.. Baada ya thanos ku-wipe nusu binaadamu wote ulimwenguni (Universe) , njia pekee iliyobakia kutimka ili kuwarudisha wale waliopotea. Probably Human can stop his Destiny which is Death, Nawaza tu labda Binaadamu twaweza kukiepuka na kukizuia kifo kwa kutumia Theory ya Time Traveling.

Time Travel ni nini..?

Ni kitendo cha kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine ndani ya muda, namaanisha kua mtu anaweza kusafiri leo hii kwenda miaka 5,10,20,25 nk ijayo (Future) au kusafiri kurudi miaka 10,20,30,40,nk iliyopita (Past). Hadithi nyingi za zamani zimekua zikielezea swala hili la kusafiri katika muda.

Huko India kuna hadithi inamzungumzia mfale Raivata Kakudumi ambae alisafiri kwenda mbinguni kukutana na mung wake Brahma, aliporudi alishangaa kua ni miaka mingi imepita. Japan pia kuna hadithi inaitwa Nihongi, inamwelezea kijana mmoja mvuvi anayeitwa Urashima taro ambae alitembelea sehemu iliyochini ya maji, baada ya siku tatu alirudi kijijini kwake akakuta ni miaka 300 imepita, alikuta familia yake imefariki yote. Pia kwa wayahudi mnamo karne ya 1BC mwanafunzi aitwae Honi ha-M'agel inasemekana ailisinzia kwa muda wa miaka 27 alipoamka alikuta hakuna mtu aliyemjua sehemu aliyokua anaishi. Na simulizi nyingii sana kuhusu hii nadharia zimetolewa waweza tafuta ukasoma zaidi.

Wakati watu wengi wakidhani kua muda hautofautiani lakini Mwanasayansi Albert Einstein anaelezea kua muda (Time) haupo hivyo wanavyodhani, unaweza kutofautiana kwa mazingira tofauti, kutegemeana na kasi unayotembea nayo angani (in space)…Theory of special relative ya Enstein inasema kua muda kwenda haraka au kwenda taratibu inategemea na kasii unavyo safiri, mtu akisafiri kwa kasi ya mwanga kwa chombo cha anga angani umri wake utakua mdogo kulinganisha na ndugu au wazazi wake aliowaacha angani..kama akirudi yeye atakua kijana lakini nduguze watakua wamezeeka au wakawa wameshafariki.

Pia kwenye theory ya Albert Einstein ya Theory of General relativity anaelezea kua Garvity (kani ya uvutano) inaweza kupeleka muda mbele au kurudisha nyuma. Anaeleza kua chombo cha anaga kikiwa huko anagani kikakutana na kani ya uvutano basi hua kani hiyo husababisha muda kua slow, hivyo basi hata wanasayansi wa anaga wanakubali kua wasafiri wa anga wanaporudi duniani hua wapo nyuma kimuda yaani saa ya duniani inakua mbele kwa muda microsecond 38 kwa siku. Wanahitimisha kwa kusema mfano msafiri mmoja wa anaga ana pacha wake duniani ammbae hafu akikaa huko angani labda siku 14, Yule pacha aliyebaki duniani atamshinda kwa muda wa microsecond 532 (chukua Microsecond 38 zidisha siku 14)



TIME MACHINE

Ili kufanikisha kusafiri katika muda inabidi kuwe na kifaa kinachoiitwa Time machine ambacho hichi kifaa kinauwezo wa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma. Bado wanasayansi wanalifanyia kazi suala hili, muda sio mrefu inaweza kuthibishwa kua Time machine inaweza kuanza kufanya kazi. Jinsi Nadharia ya Time Machine inavyofanya kazi kiukweli inanishinda kuielezea kwa Kiswahili kutokana na Ambiguity ya lugha yetu hii. Humo ni masuala ya physics tu so nashindwa niwekeje kwa lugha yetu labda aliyesoma hii kitu akaelewa inavyofanya kazi atatuelezea lifecoded.

Kwenye hili suala la tme Travel kuna kitu kinaitwa Grandfather Paradox ambapo hiki ni kitendo ambacho Time Traveller anarudi kwenye wakati uliopita kisha anaua wazazi wake au babu zake ili yeye awe hakuzaliwa.Kwa mujibu wa wanasayansi na wanafalasafa kama Plato kwenye theory yake ya Platonism anasema kua kubadili maisha yako ya nyuma hakuwezi kuathiri maisha yako ya sasa, lakini mambo yote hayo mawili yanakuja kupingwa na nadharia ya Butterfly Effectt ambapo inasema kua mabadiriko kidogo kwenye sehemu moja yanaweza kuleta mabadiriko makubwa au utofauti mkubwa baadae katika sehemu nyingine

Hii inamaanisha kwamba kama time traveler akirudi katika maisha yaliyopita akamuua baba aua babu yake anaweza sababisha mabadiriko katika maisha yake aliyotoka au future yake.

Kwa muhtsari huu kuhusu theory ya Time Traveling iko hivo japo watafiti wengi wanasema Time Travel hauwezekani iko too theoretically ila mimi naona hiki kitu ni real kabisa kipo, kwanini? Unajua binaadamu hawezi kufikiri nje ya vitu ambavyo vipo duniani nikimaanisha kua hata mimi au wewe hatuwezi kuwaza au kufikiri nje ya vile vitu tulivyoviona,kuambiwa au viliwahi kuwepo. Utawaza Mungu kwakua ulisikia kua kuna Mungu, utawaza nyumba kwakua ushaiona nyumba nk nk. Mantiki yangu ni kwamba hata hao watu wanaosema time travel is real hawakukaa tu wakafikiri kitu amabacho hakipo, mtazamo wangu naamini hiki kitu kipo na kinafanya kazi labda kwa siri kumbuka hata Internet tunaambiwa imeletwa mwaka 1991 na Tim Berners lee lakini ni kitu kipo toka miaka ya 1950s sema Tim aliifanya kua Popular baada ya kutengeneza World Wide Web…

Lakini haya ni mawazo yangu tu kwamba labada kama Time Machine ikifanikiwa kutengenezwa watu wanaweza kuitumia kukwepa kifo labda kwa kurudisha muda nyuma na kukwepa kile kitu kilichopelekea kufariki..kwa mafano kwenye muvi inaitwa Time Trveler’s wife wameelezea tukio hili linavyoweza kufanyika.
~Da'vinci..
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini