LINA MEDINA aliyezaliwa Peru mwaka 1933 ndiye msichana mdogo zaidi kuwahi kuripotiwa kujifungua mtoto.Alijifungua akiwa na miaka 5,miezi 7 na siku 21.Alizaliwa akiwa na tatizo linalojulikana kama precocious puberty ambalo humfanya mwanamke apevuke mapema. Tofauti na wanawake wengine,alianza kupata hedhi akiwa na miaka 4 tu.Nyonyo/matiti yake na nyonga vyote vilikuwa vimekomaa alipokuwa na miaka 4 tu.
Baada ya kulalamika kwa muda mrefu kuhusu maumivu ya nyonga na tumbo,wazazi wake waliamua kumpeleka hospitalini kupimwa.Hakuna aliyeamini baada ya kuambiwa binti huyu alikuwa na ujauzito wa miezi 7.May 14,1939 binti huyu alijifungua mtoto wa kiume kwa upasuaji kutokana na udogo wa nyonga zake aliyekuwa na afya bora kabisa,akiwa na kilo 2.7 ambaye walimpa jina la Gerardo kwa heshima ya jina la daktari liyemfanyia upasuaji huo.
Kama walivyo watoto wengine,Gerardo aliishi akijua Lina ni dada yake na siyo mama yake kutokana na udogo wake.Alipofikia miaka 10 ndipo alipokuja kugundua kuwa hakuwa dada yake bali mama yake mzazi.Aliendelea kuishi maisha mazuri hadi 1979 akiwa na umri wa miaka 40 alipofariki kwa kuugua ugonjwa wa saratani ya mifupa.
Lina Medina hadi sasa yupo hai akiwa amezeeka sana lakini kitu pekee ambacho aliapa kutokusema ni nani aliyempa ujauzito huo.Si baba yake,ndugu zake wala mtu yeyote yule anajua nani hasa ni baba wa mtoto wake.Kitu kingine ni kuwa,baada ya kujifungua baba yake mzazi alifungwa jela kwa kudhaniwa alimbaka binti yake lakini aliachiwa huru baada ya kugundulika kuwa hakufanya hivyo.Lina Medina yupo tayari kufanya kitu chochote ISIPOKUWA mahojiano kuhusu nani alimpa ujauzito huo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments