Zambia: Biashara za Majeneza Nje ya Hospitali Zimezuiliwa | ZamotoHabari.



Wafanyabiashara ya kuuza majeneza karibu na Hospitali ya Chuo Kikuu wametakiwa kuondoa bidhaa zao karibu na Hospitali hiyo yenye Chumba cha Kuhifadhia Maiti iliyopo Mjini Lusaka

Inasemekana kwamba, wagonjwa na jamaa zao waliwasilisha malalamishi yao katika Mamlaka ya eneo hilo na kusababisha Meya Sampa kuchukua hatua hiyo

Sampa alinukuliwa akisema, wauzaji majeneza walikuwa wanawapa wagonjwa msongo wa mawazo na kufanya iwe vigumu kwao kupata nafuu

Meya huyo pia amesema, wafanyabiashara hao wameombwa kutafuta eneo mbadala la kuuza majeneza yao au wahamishwe hadi maeneo ya makaburini kuendeleza biashara yao 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini