Zoezi la Uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Wilaya ya Tandahimba limeanza rasmi huku wananchi wakionekana kuhamasika na zoezi Hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika maeneo tofauti Wilayani hapa
Akizungumza katika kituo Cha Uandikishaji Nambahu Afisa Mwandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Tandahimba Said Msomoka alieleza kuwa amefarijika kuona wananchi wamehamasika na zoezi Hilo
Aidha aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi ili kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura
Zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Wilayani Tandahimba limeanza rasmi na linatarajia kumalizika jumapili wiki hii.
Mwananchi akiwa anafurahi kupata kadi yake ya kupiga kura
Wanachi wamejitokeza kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura
Wananchi wakisubiri kujiandikisha
Jiunge Grupu la Mishono ya Vitenge VITENGE MISHONO
0 Comments