Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema kikao kitakachomuhoji kuhusu tuhuma za kimaadili zinazomkabili kitakuwa muhimu kwake huku akitamani akitamani ushiriki wa wanahabari katika mahojiano hayo.
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyoketi Desemba 13, 2019 iliagiza makada watatu wa chama hicho waitwe na kuhojiwa na Kamati ya Maadili na Usalama ya chama hicho baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kwenda kinyume na taratibu za chama.
Membe anahojiwa leo Alhamisi Februari 6, 2020 mjini Dodoma.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam, Membe amesema ana amini kikao hicho kitakuwa kigumu huku akitumia neno ‘itategemea’, akimaanisha uamuzi utakaotolewa na kamati hiyo baada ya kumhoji.
Alipoulizwa na mtangazaji aliyekuwa akimhoji kama atakuwa tayari kwa uamuzi wowote, Membe alijibu kwa ufupi, “Itategemea.”
Kuhusu jopo litakalomfanyia mahojiano, amesema kikao hicho kitaongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, akidai mahojiano kuwa mazuri, yenye uwazi huku akitamani ushiriki wa wanahabari katika mahojiano hayo.
Baada ya mahojiano hayo, Membe amesema atakuwa tayari kuzungumza na wanahabari kwa kuwa suala hilo limekuwa wazi kwa umma tangu mwanzo.
Membe, Kinana na Makamba waliibua mjadala baada ya sauti zao kusikika mitandaoni wakizungumzia mpasuko ndani ya CCM, wameitwa sasa kuhojiwa kujibu tuhuma za kuvunja maadili.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments