Bondia Mfaume Mfaume amesema anataka kupambana na Bondia kutoka mjini Tanga, Hassan Mwakinyo muda wowote akitaka na kwa gharama yoyote anayotaka wakikubaliana.
Mfaume ameyasema hayo alipofanya mahojiano na Kipindi cha Wednesday Night cha Azam akiwa na Kocha wake, Ramadhan
Mfaume amedai pambano lake na Mwakinyo litakuwa safi sana, amesema anaamini Tanzania itasimama siku hiyo ya pambano. "Mimi binafsi natamani sana kucheza na Mwakinyo, lakini yeye ukimgusia anataja hela kubwa sababu ya hofu", amesema Mfaume.
"Mimi niko tayari muda wowote, saa yoyote kupigana naye, aseme tu anataka lini mimi nitampiga tu Mwakinyo, nina 100% mbele ya Kocha wangu nitampiga tu, yeye ni mzuri kupigana na mimi mzuri kupigana wote tupo katika Taifa moja", ameeleza Mfaume.
Mfaume amesema ili mchezo wa ngumi usonge mbele lazima Mabondia wa Taifa moja wacheze wenyewe kwa wenyewe ili mpimane uwezo na ubora katika Ngumi. Amesema ni mwaka wa pili yeye na Mwakinyo wanakimbiana amesisitiza lazima ifike hatua Watanzania wapate radha ya mchezo wa ngumu kwa wao kukutana ulingoni.
"Siku nyingi sana namtafuta Hassan Mwakinyo, saa yoyote, muda wowote mimi niko tayari kupigana naye, aje tu yeye Bondia mzuri lakini mimi mzuri ziadi yake", amedai Mfaume.
Kwa upande wake, Kocha wa Mfaume Mfaume, Ramadhan amesema kama Hassan Mwakinyo atakubali ilo pambano, lazima atapigwa na Bondia Mfaume Mfaume, "Naamini Mfaume ni Bondia bora sana katika Taifa hili, Mwakinyo lazima atapigwe", ameeleza Ramadhan
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments