MSANII wa filamu nchini Jacqueline Wolper, amesema amewakumbuka wale wanaume wa zamani ambao walikuwa wanawahonga wanawake magari na nyumba na sasa imepita miaka miwili bila kusikia fujo zao.
Kupitia mtandao wa Instagram, msanii huyo wa filamu amepost video fupi yenye dakika moja, ambayo anamuomba Mungu awarudishie wanaume hao wa zamani wenye tabia hizo.
“Nina miaka kama miwili hivi zile fujo za waya sizisikii, kama mwanaume kamnunulia gari la IST mwanamke wake basi anatokea pedeshee anamwambia mtoto mzuri kama wewe hufai kutembelea gari hilo la misaada na kupeleka watoto shule, halafu yeye anakupa Range Rover,” amesema Jacqueline Wolper.
Aidha ameendelea kusema; “Hata ukisema unakaa Sinza anakwambia uhamie Masaki, Mungu na Yesu naomba uturudishie wale wanaume wa zamani waliokuwa wanatuhonga Range Rover”.
Pia, Jacqueline Wolper amekiri kwamba, amewahi kudanga kwa kuwa na mwanaume mwenye pesa ili kusaidia kuendeleza maisha yake.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments