Na Bartholomew Wandi
Wapiga Kura wa Kata yaKibuta, iliyoko Halmashauriya Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani wameombwa kujitokeza tena kwa wingi katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura ili taarifa zao zilizochukuliwa kwenye zoezi la majaribio ziweze kuingizwa rasmi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tumeya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (R) Mbarouk Salim Mbarou kwa kati wa Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi wa Mkoa wa Pwani.
Wadau hao wa Uchaguzi waliokutana na Tume Mkoani Pwani ni Viongozi wa Vyama vya Siasa,Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wawakilishi wa makundi maalum ya Watu wenye Ulemavu, Vijana, Wanawake, Wanahabari na Wazee wa Kimila.
MakamuMwenyekitialisemaUboreshajiwaMajaribiokwa Kata yaKibutana Kata ya Kihondaulifanyika kuanzia tarehe 29 Machi 2019 hadi tarehe 4 Aprili, 2019, na dhumuni lake lilikuwa ni kupima uwezo wa wa mfumo wa uandikishaji na utendaji kazi wa vipuri vipya vilivyofungwa kwenye mashine za kieletroniki za Biometriki (BVR).
Jaji Mbarouk aliwafahamisha Wadau hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekamilisha maandalizi kwa ajili ya zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kundi la Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, linatarajiwa kufanyika kwa siku 7 kuanzia Februari 14 hadi 20 mwaka huu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na Vituo vya Uboreshaji vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
Kwa Mkoa wa Pwani,idadi ya Vituo1,734vya kuandikishia Wapiga Kura vilivyokuwepo mwaka 2015 ni idadi hiyo hiyo1,734 ya vituo itakayotumia mwaka mwaka 2020 ila kwa nchi nzima vituo vitakavyotumika kuandikisha Wapiga kura vimeongezeka kutoka 36,549 mwaka 2015 hadi Vituo 37,407 mwaka 2020.
Aidha, Makamu Mwenyekiti wa Tume alibainisha kuwa, mikoa ishirini na nane (28) ya Tanzania Bara na Zanzibar imekamilisha zoezi hili tangu kuzinduliwa kwake mnamo tarehe 18 Julai, 2019 huko katika Mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk aliitaja mikoa hiyo 28 iliyomaliza zoezi hilo kuwa ni Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Simiyu, Mara, Mwanza, Kigoma, Tabora, Songwe, Kagera, Geita, Shinyanga, Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Tanga na Morogoro kwa Halmashauri za Wilaya za Ulanga na Malinyi kwa Tanzania Bara na kwa Tanzania Zanzibar ni mikoa ya Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja na Mjini Magharibi.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments