Tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi ZAMOTOHABARI APP. Sasa ipo Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.
Moja ya vyumba vya kituo cha ununuzi wa madini kilichopo ndani ya Mgodi wa Almasi wa Williamson mkoani Shinyanga kitakachotumika kwa ajili ya kununua asilimia tano ya madini ya almasi katika mgodi huo.
…………………………………………………………………………………
Waipongeza Serikali…
Na Greyson Mwase, Shinyanga
Wafanyabiashara wadogo wa madini ya almasi mkoani Shinyanga wanatarajia kuuziwa asilimia tano ya almasi inayochimbwa na Mgodi wa Almasi wa Williamson kama njia mojawapo ya kuwainua kiuchumi na kuimarisha masoko ya madini yaliyopo mkoani Shinyanga.
Akizungumza na wanahabari kutoka Idara ya Habari MAELEZO tarehe 06 Februari, 2020 kweye kituo kipya kilichoandaliwa kwa ajili ya kuuzia madini hayo mkoani Shinyanga, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu alisimulia kuwa kupitia mkutano wa wadau wa madini na Waziri wa Madini, Doto Biteko uliofanyika mapema Julai mwaka jana, wafanyabiashara wadogo wa madini waliomba kuuziwa asilimia tano ya madini ya almasi na Mgodi wa Williamson kama njia mojawapo ya kuimarisha biashara ya madini hayo na kujiongezea kipato huku Serikali ikipata kodi mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Kumburu alisema Serikali inaandaa utaratibu wa kugawa makinikia yaliyokuwa yanamilikuwa na Mgodi wa Williamson kwa wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kuyachenjua na kupata madini kwa ajili ya kuyauza.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wa madini katika mkoa wa Shinyanga, Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoani Shinyanga, Gregory Kibusi aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa hatua iliyochukua katika kuhakikisha wachimbaji wananufaika na rasilimali za madini.
Alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini, wafanyabiashara wa madini mkoani Shinyanga wamekuwa wakiuza madini yao kwa uhuru na kulipa kodi mbalimbali Serikalini huku ulinzi ukiimarishwa kwenye masoko ya madini.
Katika hatua nyingine, Kibusi aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuacha utoroshaji wa madini na kuanza kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa.

Tunakushauri kutumia APP yetu ili kusoma kwa urahisi ZAMOTOHABARI APP. Sasa ipo Playstore, ili ku-download BOFYA HAPA.Alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ilifanya mawasiliano na Mgodi wa Williamson ambapo ilikubaliwa kuanza kwa mchakato ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha awali kitakachotumika kwa ajili ya kuuza madini husika kwa wafanyabiashara wadogo wa madini kwa njia ya mnada.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Kumburu alisema Serikali inaandaa utaratibu wa kugawa makinikia yaliyokuwa yanamilikuwa na Mgodi wa Williamson kwa wachimbaji wadogo wa madini ili waweze kuyachenjua na kupata madini kwa ajili ya kuyauza.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wa madini katika mkoa wa Shinyanga, Katibu wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoani Shinyanga, Gregory Kibusi aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa hatua iliyochukua katika kuhakikisha wachimbaji wananufaika na rasilimali za madini.
Alifafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa masoko ya madini, wafanyabiashara wa madini mkoani Shinyanga wamekuwa wakiuza madini yao kwa uhuru na kulipa kodi mbalimbali Serikalini huku ulinzi ukiimarishwa kwenye masoko ya madini.
Katika hatua nyingine, Kibusi aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuacha utoroshaji wa madini na kuanza kutumia masoko ya madini yaliyoanzishwa.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments