Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu amewaonya wafanyabiashara wa Tanzania wanaoingiza wanaoendelea kuingiza mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku nchini.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Februari 8, 2020 Itigi Wilaya ya Manyoni Mkoa wa Singida wakati akiteketeza tani 11.53 za mifuko ya plastiki iliyokamatwa katika Mikoa ya Singida, Tabora na Dodoma kuanzia Juni hadi Desemba 2019.
Amesema Serikali imeshapitisha sheria ya kuzuia matumizi ya mifuko hiyo nchini kwa kuwa ina madhara kiafya lakini kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaovunja sheria na kuingiza mfuko hiyo iliyokatazwa.
“Nipende kutoa rai Serikali imeshatoa agizo na sheria imeshatungwa, mifuko hii ilipotea imeshaanza kurudi inarudi kwa sababu wafanyabiashara wamekuwa na kiburi cha kufanya shughuli hizi kwa kudharau mamlaka.”
“Lakini tuwaonye wananchi mifuko ambayo haina viwango na ambayo haikuruhusiwa kisheria ina athari za kiafya ni michafu na inatengenezwa bila kusimamiwa ubora wake na vyombo vilivyowekwa kisheria hivyo ni hatari kwa mazingira na afya zao,” amesema Zungu.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments