Na Editha Karlo,Kigoma
FAMILIA ya wasomi wa Chama cha mapinduzi(CCM) mkoani kigoma wanazuoni wametoa tamko juu ya kitendo alichokifanya mbunge wa kigoma mjini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe cha kupeleka maombi ya zuio la mkopo kwa serikali ya Tanzania bank kuu kwaajili ya kuboresha Elimu.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Mkoa za chama cha mapinduzi wanazuoni hao wamesema kuwa jambo alilolifanya Zitto halikubaliki na ni kitendo kisichoungwa mkono kabisa na wanakigoma na hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.
Kwa Habari za Uhakika na Haraka pakua APP yetu. ZAMOTOHABARI: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP mpya. Ukitaka kudownload kupitia Playstore tafadhali BOFYA HAPA."Kitendo alichokifanya Zitto siyo kitendo kizuri kwasababu Zitto ni mbunge kwani ana uwanja mkubwa wa kuzungumza hayo bungeni nasiyo kuandika barua binafsi yeye kama zitto ya kuzuia fedha za mkopo wa kuboresha elimu toka bank kuu"alisema Eliya Michael mwana CCM na mwanazuoni wa Mkoa wa Kigoma
Eliya alisema kuwa Zitto anapaswa kukemewa kwa jambo alilolifanya kukaa kimya watu wataona jambo alilolifanya ni sahihi lakini wao kama wanakigoma wanasema alichokifanya zitto hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.
Naye William Mtula mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa watanzania kuungana pamoja na kumtia moyo Rais kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi.
Mtula alisema kuwa matakwa ya Watanzania nikupata huduma bora na za msingi kama vile elimu,afya,miundombinu na zingine.
"Zitto ni mbunge pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kigoma mjini bungeni hivyo alipaswa kuongelea hoja za wananchi wake na kero zilizopo jimboni kwake na sihayo aliyoyafanya dhidi ya serikali yake"alisema
Wanazuoni hao wamewataka wananchi wa jimbo la Kigoma mjini kulitafakari hilo na kuona sasa ni wakati wao wa kutafuta mwakilishi ambaye atawawakilisha vizuri na siyo yule anayefanya kazi amabazo wananchi hawajamtuma.
Mwanazuoni na mwanachama wa chama cha mapinduzi(CCM)Eliya Michael akiongea na waandishi wa habari juu ya barua ya Zitto Kabwe kwenda bank kuu kwaajili ya kusitisha mkopo wa elimu kwa serikali
Baadhi ya wasomi wa chama cha mapinduzi(CCM)wa mkoa wa Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya tamko lao kwa mbunge wa kigoma mjini Zitto Kabwe
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments