Watu Wengine 41 Wambukizwa Corona Katika Meli ya Japan | ZamotoHabari.


Uchunguzi kuhusu virusi vya corona umebainisha kuwa idadi nyingine ya watu 41 waliokuwemo katika meli ya safari za starehe ya kijapani wamebainika kuwa na maambukizi.

Taarifa hizo ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan, likiwemo shirika la habari la umma wa taifa hilo NHK.

Visa hivyo vinaongeza idadi ya maambukizi kufikia watu 61 kwa meli hiyo inayofahamika kama "Diamond Princes". Hadi wakati huu idadi ya vifo itatajwa kupindukia watu 600, na wengi wa hao ni kutoka China ambako virusi hivyo vinaelezwa kuanzia kuzuka.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini