Yanga Yaendelea Kumfukuza Mwizi Kimya Kimya.... | ZamotoHabari.



Yanga Africa yaendelea kumfukuza mwizi kimya kimya maara baada ya leo kuendelea kugawa vipigo mfululizo dhidi ya wazee wa kupapasa Ruvu Shooting ya Mlandizi Mkoani Pwani.

Yanga ilitumia dakika 40 za mchezo katika kipindi cha kwanza kupata bao la kuongoza na la ushindi katika mtanange huo mkali mara baada Papaa Davido Molinga kumalizia kwa kichwa krosi iliyopigwa na Ditram Nchimbi na kumshinda mlinda mlango wa Ruvu Shooting Mohamed Makaka.

Yanga sasa wanajikusanyia alama 37 katika michezo 18 ya ligi kuu Tanzania bara huku ikishika nafasi ya tatu nyuma ya vinara wa ligi wekundu wa msimbazi we alama 50 katika michezo 20.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini