Burkina Faso yaripoti kifo cha kwanza cha Corona 'Sub-Sahara', virusi hivyo vyaua karibu 500 Italia ndani ya saa 24 | ZamotoHabari.

Waathiriwa wa kirusi cha corona nchini Kenya wamefikia watu saba baada ya watu wengine watatu kuthibitishwa kuambukizwa kirusi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema kuwa, watu wote hao saba wametoka nje ya Kenya. Wawili kati ya wagonjwa hao watatu wa karibuni kabisa wametokea Madrid Uhispania kupitia Dubai na mgonjwa wa tatu ni raia wa Burundi aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akitokea Dubai pia.

Huku hayo yakiripotiwa, Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imetangaza kuongezeka idadi ya waathiriwa wa kirusi cha corona nchini humo na kufikia watu 85 ikiwa ni ongezeko la watu 34 ikilinganishwa na taarifa ya kabla yake.

Kabla ya hapo Wizara ya Afya ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza kuwa watu 51 wameambukizwa kirusi cha corona nchini humo.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini