Corona yaua DRC na Mauritius, Algeria yafuta maandamano | ZamotoHabari.

Mgonjwa wa corona ameaga dunia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hicho kikiwa ni kifo cha kwanza kilichosababishwa na ugonjwa huo nchini humo, huku kesi za maambukizi ya kirusi hicho barani Afrika zikiendelea kuongezeka.

Waziri wa Afya wa DRC, Eteni Longondo amethibitisha hayo katika ujumbe wake kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter jana Jumamosi, sanjari na kutangaza kesi tano mpya za wagonjwa wa Covid-19 nchini humo.

Aidha jana Jumamosi, Mauritius ilisajili kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona nchini humo, huku idadi ya watu walioambukizwa kirusi hicho ikiongezeka na kufikia watu 13.

Nchini Algeria watu wasiopungua 12 wameaga dunia kutokana na corona na wengine karibu 100 wanasumbuliwa na virusi hivyo, jambo ambalo limepelekea kufutwa kwa maandamano ya kila wiki dhidi ya serikali kwa mara ya kwanza tokea Februari 2019, wakati aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika alipotangaza kuwa atagombea muhula wa tano wa urais.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini