Coronavirus: Jimbo la California lawaamuru watu kubaki nyumbani kudhibiti maaambukizi | ZamotoHabari.

Jimbo la California limewaamuru wakazi wake "kukaa nyumbani" huku likijaribu kudhibiti maambukizi ya coronavirus katika jimbo hilo maarufu zaidi nchini Marekani.

Govana Gavin Newsom aliwaambia wakazi wa California kuwa watatakiwa kuondoka majumbani mwao tu wakati ni muhimu wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.

Awali alikadiria kuwa zaidi ya watu milioni 40 katika jimbo lake wanaweza kupata maambukizi ya virusi vya Covid-19 katika miezi miwili ijayo.

Virusi vya corona tayari vimewaua watu 205 nchini Marekani huku watu 14,000 wakipata maambukizi.

Kwa ujumla wagonjwa karibu 250,000 kote duniani wamepatikana na virusi hivyo vinavyosabisha ugonjwa kupumua na takriban 9,900 wamekufa.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini