Abiria kwenye meli ya kifahari ya MS Zaandam iliyopewa jina la ‘Death ship’ yenye watu walioambukizwa Virusi vya Corona na ambayo imekwama nchini Panama, wameambiwa kwamba bado kampuni inayomiliki meli hiyo inatafuta bandari itakayokubali kuwapokea, siku kadhaa baada ya kutuma maombi maalum ya msaada.
Coronavirus Australien Fremantle Kreuzfahrtschiff Artania soll Gewässer verlassen (Getty Images/P. Kane)
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Kampuni ya Holland America Line, Orlando Ashford, baada ya meya wa mji mmoja wa jimbo la Florida nchini Marekani kusema kuwa hawako tayari kuipokea meli hiyo.
Orlando amewaambia abiria hao kupitia ujumbe wa video kuwa bado wanajaribu kuangalia mahala pa kuwashusha, huku watu wanne ndani ya meli hiyo wakiwa wamefariki kutokana na ugonjwa COVID-19 na huku wengine baadhi wakiwa wameathirika.
“Tumekwama katika meli hii ya kifo ‘death ship’, amesema mmoja wa abiria ambaye yupo na mumewe katika meli hilo la kifahari.
“Tumechoshwa, nataka kutoka, tunaogopa kwamba na sisi tutakuja kuambukizwa pia. Kama tutaendelea kukaa ndani ya meli kuathirika ni swala la muda tu.” Akiongea kwa majonzi abiria huyo.The cruise ship MS Zaandam off the coast of Panama City. Photo: Reuters
Meli hiyo ya kifahari iitwayo Zaandam imekwama kwenye Bahari ya Pasifiki tangu tarehe 14 mwezi huu wa Machi, baada ya baadhi ya watu miongoni mwa abiria wake 1,800 kuanza kuuguwa ugonjwa wa mafua, na bandari kadhaa za Amerika Kusini kuikatalia kutia nanga.
Daktari wa meli hiyo ameripoti kuwa mpaka sasa asilimia 40 ya wafanyakazi ni wagonjwa, huku akiwataka abiria kujiweka karanti.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments