"Harusi wiki ijayo" - Hamisa Mobetto Afunguka | ZamotoHabari.


Baada ya kusema yupo single kwa muda mrefu sasa, mrembo na msanii Hamisa Mobetto amekiri na kuweka wazi kuwa yupo tena kwenye mahusiano na ndoa yake inaweza ikawa wiki ijayo.


Hamisa Mobetto ameeleza hivyo kupitia insta story ya mtandao wa Instagram, ambapo alitoa muda kwa mashabiki zake kumuuliza maswali yoyote kisha yeye kutoa majibu.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa yalikuwa ni bado upo single, shemeji yetu ni nani, na harusi yake ni lini ambapo amejibu kwa kuandika,

"Sijarudiana na EX wangu na sipo single, nipo kwenye mahusiano sasa hivi, ila nina shemeji yenu mzuri, siku ya ndoa mtamuona inshaalah na harusi wiki ijayo".

Pia kupitia mitandao ya kijamii kuna stori ambazo zinaeleza kuwa huenda Hamisa Mobetto na Alikiba wamefikia hoteli moja huko visiwani Zanzibar, baada ya ramani "location" zao kusoma zipo sehemu moja hali ambayo inafanya watu kuwaza vitu tofauti.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini