Hospitali ya Kenya yapokea Mgonjwa Mwenye Corona | ZamotoHabari.



Wizara ya Afya nchini Kenya imetoa taarifa ya kuwepo kwa mgonjwa wa kwanza mwenye virusi vya wa corona.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, mgonjwa huyo raia wa Kenya alithibitishwa kuwa na virusi hivyo baada ya kurejea nchini kutoka Marekani, Alhamisi, Machi 5.

Mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH).

Waziri ameripoti kuwa, mgonjwa huyo wa kike anaendelea vizuri na matibabu na kwamba joto lake la mwili limepungua.

Mikutano yote ya hadhara, kutembelea wafungwa vimepigwa marufuku kwa sasa na wizara imewataka Wakenya wote kuzingatia usafi wakati wowote.

Mpaka sasa jumla ya nchi 155 zimeripotiwa kuwepo kwa virusi vya Corona.


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini