Italia yavunja tena rekodi, watu 793 wafa siku moja kwa corona, Ulaya yazidi kulemewa na vifo na maambukizi | ZamotoHabari.

Kwa mara nyingine tena Italia imevunja rekodi ya watu wengi zaidi waliokufa siku moja kutokana na maambukizi ya kirusi hatari cha corona kiasi kwamba katika kipindi cha masaa 24, watu 793 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini humo.

Shirika la ha habari la Tasnim limelinukuu shirika la habari la AFP likitangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Wakala wa Kuwalinda Raia wa Italia ulisema jana kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na kirusi cha corona nchini humo ilikuwa ni 793 katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita na hadi kufikia jana watu 4800 walikuwa wameshafariki dunia nchini Italia kutokana na kirusi hicho.

Wakala huo wa kulinda raia nchini Italia pia umesema, hadi kufikia jana karibu watu 53600 walikuwa wameshaambukizwa ugonjwa wa COVID-19 ikiwa ni ongezeko la watu 6500 ikilinganishwa na tangazo lililotolewa juzi Ijumaa.

Italia hivi sasa ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na imeipiku hata China ambayo vyombo vya habari vya Magharibi vinadai ndiko ulikoanzia ugonjwa huo. Hadi hivi sasa watu 3,255 wamefariki dunia kwa ugonjwa huo nchini China.
 


APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini